The Extent You Know The Truth,
The Extent You will Enjoy Salvation

kiango media

kiango media

Advertisement

Advertisement

Pages - Menu

Tuesday, October 21, 2014

Wanamuziki wa Injili Kenya Wajitokeza Kuchangia Baba Yao Wa Kiroho Kimuziki

Baba wa Kiroho wa wanamuziki wengi wa Injili nchini Kenya Bishop Ben Bahati ambaye alipata ajali ya gari wakati akitoka katika Mji wa Nakuru kwenda Eldorate. Bishop Ben ambaye alipata ajali chache mita chache kabla ya kufika nyumbani kwake kwa sasa amelazwa katika hospitali ya Nairobi.

Kutoka na ajali hiyo Wanamuziki Wa Injili Nchini Kenya na Watu wadau wa Muziki wa Injili nchini humo wameanzisha harambee maalum kwa ajili ya Kusaidia matibabu ya Bishop Ben ambaye ni Mdau Mkubwa wa Muziki wa Injili. Hali ya Bishop Ben kwa siku kadhaa imekuwa si njema sana ingawa amekuwa akipata matibabu kutoka katika hospitali hiyo.
Mmoja kati ya Watu waliojitokeza ku-support gharama hizo ni Celebrate wa Kenya mwenye jina la Jaguar ambaye ametoa shilingi Millioni 4 za Kenya ili kusaidia Bishop huyo kupona haraka. Harambee ya "Simama na Ben" imekuwa na mwitikio kutoka kwa "Wakristo" na Wasio "Wakristo".

Papaa On Tuesday....Siku Njema Haziongozani, Zikiongozana Hazirudii Tena....

Tukiwa tumebakiza siku chache ili tuingie Mwaka 2015 kila mtu ana jambo la kusema kuhusu mwaka huu wengine wana kila sababu ya kuwa meno nje sababu katika mwaka huu kunajambo kubwa la mafanikio limetokea kwenye maisha yao, wakati huo huo wako ambao mwaka huu wamefurahi wakalia wakafurahi, wakalia so ni kama 50-50 kwao na wapo wale ambao wanatamani mwaka huu wauongeze speed uishe haraka maana huu mwaka kwao umekuwa mwaka wa kumbukumbu zisizo njema kwao na Wakasahau kama ambavyo siku njema haziongozi basi 
pia
 hata siku mbaya haziongozani.


Mwaka 2012 niliandika Papaa On Tuesday yenye episode one ya Title hii kuhusu Kutokujirudia kwa siku njema. Katika Makala ile nilieleza kuwa msemo huu Mama alikuwa akiutumia sana tulipokuwa watoto wakati ambapo familia ilikuwa inapita kwenye majira ya neema na furaha sana wakati ambapo tulikuwa tunakula na kusaza, tunakunywa na kumwaga basi mama alikuwa anatuambia "Siku Njema Haziongozani, Zikiongozana Hazirudii tena". Ilipotokea siku tunapita kwenye magumu na kuwaza machungu tuliyonayo Mama alikuwa anatukumbusha nyakati zile tulizokuwa na furaha na kusema "Hata Hili Nalo Litapita".
Kuna Changamoto nyingi sana tumepitia mwaka 2014 na kwa siku chache zimebaki tutaendelea kuwa na changamoto mbali mbali na kila mtu anatamani kuanza a new page ya mwaka 2015 kwenye Calender zetu ili tuweze kusahau na kuukabili mwaka mpya lakini cha kujiuliza unasubiri kalenda ili ujipange??Mwanzoni mwa mwaka huu niliandika ukiona unajipanga ujue ulipanguka, sasa lini kwako ni tarehe muafaka ya kujipanga baada ya kupanguka. Rafiki yangu Mussa Billegeya  aliwahiniambia Hakuna jambo la Maana kama Mungu kuuanza Mwaka Mpya Wako na Kufungua a New Page aiseee kila kitu kwako kitakuwa kipya, wakati huku tukifungua kalenda mpya usiombe Mungu akafungua kalenda yako ya mwaka mpya kila mtu atatamani kusoma tarehe zako na kustawi kwako.

Mwaka 2014 mimi binafsi na yamkini ndugu msomaji tumepita kwenye nyakati ambazo tulitamani kukaa wenyewe tu na kuliaaa na kutafakari pasipo kutaka kuteta na mwanadamu yeyote kwa sababu ya yale maumivu ya nafsi tuliyokuwa nayo nyakati hizo. Katika Mwaka huu kuna mambo yameacha alama katika akili zetu, kuna mambo yameacha makovu katika mioyo yetu kuna mambo yameacha kumbukumbu isiyooza kwenye nafsi kiasi kwamba tulitamani masaa ya siku hizo yakomeshwe. Mwaka huu kuna nyakati pia tulikuwa na wakati tulikuwa na rahaaa mpaka tukadhani hakuna Kufa na hata kama kifo kingetokea tungedhani hatukustahili nyakati hizo kufa siku njema ziliongozana sana kwetu kiasi kwamba nyimbo na mawazo yalikuwa yanaonesha kabisa maisha ni matamu na tukasahau kuwa Siku Njema haziongozani na Zikiongozana hazirudii tena.
Kuna baadhi ya Watu ninawafahamu mwaka huu wamepata hasara ya biashara zao, kuna watu mwaka huu wamepoteza wenzi wao kuna watu mwaka huu wameshindwa kulipa ada za shule, kuna watu mwaka huu wameona ama walihisi wana deserve Kufa kuliko kuishi kila kitu kwao kimekuwa "mwaka wa shetani" na kusahau hakuna linalodumu katika maisha maana hata hilo nalo litapita, halijalishi ukubwa wake lakini lakini Mungu akiamua kukupa kicheko sio lazima aanze kukupa tabasamu kwanza. 

Kuna watu wamelalamika sana kuwa mishahara yao haitoshi, ndoa zao zimekuwa za kusua sua, maisha yamekuwa ya madeni hakuna siku wamekopesha kila wakitoa fedha kwa mtu ilikuwa ni kwa ajili ya kulipa madeni na si kukopesha, wengi wetu usiku ulikuwa mrefu kwa kuingoja asubuhi ifike tutoke nje, yamkini ni mwaka ambao umetoa machozi baada ya muda mrefu kupita kutoyatoa, yamkini ndio mwaka ambao umebaini umepata ugonjwa wa pressure yamkini ndio mwaka uli experience kudhalilishwa kwenye maisha lakini jua jambo moja HATA HILO NALO LITAPITA.

Yaliyopita tuyaache yapite tugange yajayo, maana Biblia inasema Mungu anatuwazia mawazo ya amani kuliko wanadamu Mungu anawaza Kutupa Tumaini siku zetu za Mwisho, hata usiku ukiwa na giza totoro namna gani asubuhi itafika, hata mlima ukiwa mrefu namna gani lakini upande wa pili wa Mlima ni Mteremko. Huwezi kuwa wewe ni wakushindwa siku zote sisi ni washindi zaidi ya washindi kwenye maisha yetu..

Siku Njema haziongozani na siku mbaya pia hazidumu, katika kila Jaribu kuna Mlango wa Kutokea, mateso ya mwenye haki ni MENGI lakini Bwana humponya nayo YOTE.

Think Differently and Make a Difference.

Papaa Ze Blogger
0713 494110